TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam 16.4.2012: Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania imepunguza gharama zake za
kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20 ambapo
mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala yeyote wa m-pesa. Gharama hizi
zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw.
Rene Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa
wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia
zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya
Vodacom M-PESA .
“Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa
ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo
tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ”, alisema
Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za
kutoa fedha. ‘Hili ni lengo letu muhimu
mwaka huu na zaidi” alisisitiza Bw. Meza.
Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya Kampuni kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa
ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya
siku 90 iitwayo ‘tuma na ushinde’ ambapo shilingi milioni 480 zitashindaniwa
kwa kipindi chote cha promosheni.
Jukumu letu ni
kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na
huduma zetu ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili
kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya
kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.
Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na
malipo ya bili kama vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA.
Vilevile inaweza kutumika kulipia
tiketi, safari za ndani za
ndege za Precision Air na Coastal ,
ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za shule, kuweka na kutoa fedha kupitia
Benki ya CRDB, Western Union na huduma zingine nyingi.
Vodacom m-pesa ina
mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka kwamba
Vodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na matumizi ya
kuongezeka siku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa
masuala ya fedha hapa nchini.