MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa
filamu nchini marehemu Steven Kanumba amewataka wasanii wanachama wa
Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha
mwanae.
Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na (SHIWATA) leo Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi.
"Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa ipendo na ushirikiano mlionesha kwa familia yangu, naomba muendeleze ushirikiano mliokuwa nao wakati mwanangu akiwa nanyi, endeleeni kushirikiana" alisema Mama Kanumba.
Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji wa Kanisa la Elim Pentekoste Ilala Bungoni, Mchungaji Livingstone Mwaitela alisema wasanii na familia ya Kanumba wasisononeke kwa sababu Mungu alimpenda
mtoto wao huyo zaidi.
Alisema wasanii waendelee kumkumbuka mwenzao kwa kubadili mambo yasiyompendeza Mungu badala yake wajiandae kwa kufanya mambo ambayo yanampendezesha na kujiweka tayari siku akiwaita wawe tayari.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema Kanumba alikuwa mwanachama wao namba 648 akiwa mmoja wa waliojitokeza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba za wasanii kutoka Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo Mkuranga.
Marehemu Kanumba alifariki Aprili 5, wakati akikimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka nyumbani kwake Sinza kufuatia ugomvi wa mapenzi na msanii mwenzake Elizabeth Michael (Lulu).