Baada ya historia ndeeeefu ya kutowaona kwa macho 50 Cent na Oprah Winfrey wakiwa pamoja, nyota hao wamepanga kusuluhisha ugomvi wao kwenye episode mpya ya kipindi cha Oprah’s Next Chapter kinachorushwa kwenye kituo chake cha runinga cha OWN.
Akionesha kwa ufupi itakavyokuwa leo, Oprah anaonesha kufurahia muda wa pamoja na 50 na amefurahi sana kulimaliza beef lao.
“Ni mazungumzo mazuri kuhusu utamaduni wa rap, ubaba, mapenzi na maisha,” alisema. “Anajieleza mwenyewe kama watu wawili Curtis na 50 Cent — Nilifurahishwa kusikia maelezo ya watu hao tofauti. Nimefurahi nimefanikiwa. Kanifurahisha.”
Interview hiyo ilifanyika kwenye nyumba ya Bibi yake na 50.
Beef ya Oprah na 50 ilianza tangu mwaka 2006 baada ya kumshutumu kuwa na ubaguzi dhidi ya wasanii wa Hip Hop kwenye show yake. 50 Cent alisema show ya Oprah ilikuwepo kwaajili ya wanawake wazee wa kizungu na ndio maana alikuwa haipendi.
Kutokana na kumchukia Oprah, 50 aliamua kumpa jina hilo mbwa wake.
Mwezi March mwaka huu rapper huyo mwenye scandal kibao alihojiwa kwenye show ya “The View” inayoendeshwa na Whoopi Goldberg, Joy Behar, Elisabeth Hasselbeck na Sherri Shepherd na kuzungumza kuhusu mapenzi, utoaji wa misaada na mbwa wake Oprah.
“Ilianza kwasababu nilihisi Oprah haupendi utamaduni wa hip-hop,” alisema Fif. “Mbwa yupo na sasa nampenda Oprah.” (Rap-Up)
Oprah ataongea pia na binti yake na Michael Jackson, Paris katika episode hiyo mpya itakayorushwa saa 3 usiku muda wa Marekani.