Jambo limezua jambo mjini! Siku chache baada ya kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli, Steven Charles Kanumba ‘The Great’ huku mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa nyuma ya nondo za Segerea, Dar kuhusiana na kifo hicho, mtaani wameibuka watu wawili wanaofanana na mastaa hao na kusababisha gumzo kubwa, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili hivi karibuni zilieleza kuwa kuna binti aliyetajwa kwa jina la Yolanda Michael (Lulu fotokopi, pichani), mkazi wa Tip Top jijini Dar ambaye amefanana na Lulu na amekuwa akipata wakati mgumu anapokatiza mitaani akihisiwa ni Lulu halisi.
Mwanzoni Risasi Jumamosi halikuamini maneno ya mitaani, hivyo kwa nyakati tofauti, mapaparazi wetu waliwatafuta watu hao na kuwaweka kwenye mizani ambapo picha zao zilibainisha kufanana kwa asilimia nyingi (tazama ukurasa wa mbele).
BOFYA HAPA KUMSIKIA YOLANDA!
Akihojiwa ‘exclusively’ na mapaparazi wetu, Yolanda, binti wa miaka 18 aliweka wazi kuwa mara kadhaa amenusurika vipigo kutoka kwa watu ambao walitaka kumuadabisha wakidai kuwa yeye ni Lulu (Elizaberth Michael) wakimtuhumu kwa kifo cha Kanumba.
MAJINA YA BABA ZAO
Pia, jina la baba yake ni Michael kama lilivyo la baba wa Lulu orijino (Michael).
HEBU MSIKIE KANUMBA FOTOKOPI
Akizungumza na paparazi wetu katika ofisi za gazeti hili, Thadei Pius Michael (jina kama la baba Lulu na Yolanda), ambaye ukimuoana huulizi kwa jinsi alivyofanana na marehemu Kanumba, amekuwa akipata wakati mgumu kwa watu wanaopita katika eneo lake la kazi ya ufundi gereji.
“Baada ya kifo cha Kanumba ndiyo hali imekuwa mbaya zaidi kwani watu wakiniona wanadhani ni mzimu wa marehemu Kanumba.
“Wengine wamekuwa wakinizunguka na kunikagua kwa kunitazama hali ambayo inanikosesha amani.”
Baadhi ya wananchi waliozungungumza na gazeti hili, walidai walishindwa kuamini kutokana na jamaa alivyofanana na The Great kuanzia midomo, macho, pua, urefu na baadhi ya sehemu nyingine za mwili.
CHANZO GLOBAL PUBLISHER