Uchunguzi uliofanywa na Mpekuzi umebaini kuwa Diamond anaingiza kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 16 kwa kila shoo mbili anazofanya akiwa ndani na nje ya jiji la Bongo.
“Nashukuru Mungu kwa kufika hapa na ukweli ni kuwa nalipwa mkwanja huo na hii imekuja kufuatia kuweka nguvu zangu katika muziki na kufanya vitu vizuri kwa kuwa gemu ndiyo maisha yangu” alisema Diamond.
Akiendelea zaidi nyota huyo wa ‘Songi’ la ‘Mawazo’ alianika kuwa mafanikko haya yanakuja pia kutokana na sapoti anayoipata kutoka kwa watu wake wa karibu akiwemo Mama yake mzazi na wengine kibao.
Hapa chini ni mkataba ambao amelamba kutoka kampuni ya Emilates Hall kupiga shoo huko pande za Mtwara