Shakoor Jongo na Erick Evarist
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa (pichani) juzikati alijikuta akiangua kilio upya wakati alipokuwa akipokea shilingi milioni 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla kama rambirambi kutoka serikalini.
Akikabidhi fedha hizo, Mhe. Makalla alisema serikali imefikia hatua hiyo kutokana na mchango mkubwa wa marehemu Kanumba kwa jamii na serikali kwa ujumla enzi za uhai wake.
“Mimi sikubaliani na hilo kwani katika watu waliokuwa wakihamasisha kufunguliwa kwa tawi la CCM nchini Uingereza, marehemu alikuwa miongoni mwao na ndiyo urafiki wetu ulipoanzia,” alisema Makala.
Alisema tangu mwanaye huyo afariki dunia amekuwa ni mtu wa kulia kila siku huku akiamini kuwa, atakuwa ni mtu wa kufuta machozi kwa siku 365.
“Naishukuru sana serikali kwa rambirambi hii lakini kwa kweli kila ninapokumbuka kifo cha mwanangu, machozi hayaishi kunitoka, itanichukua muda kusahau,” alisema Mama Kanumba.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS