MISIMAMO YA ROMA ILIMFANYA AFUKUZWE SHULE


Ibrahim Musa aka Roma kama watu wanamvyomtambua, hakuanza leo hii kuwa na misimamo mikali dhidi ya utawala.
Msimamo mkali ulimcost masomo pamoja na wenzake kadhaa baada ya kufukuzwa shule alipokuwa katika shule ya Sekondari ya Old Moshi.


Hatua hiyo ilimfanya Roma ambaye jina lake hilo kwa mujibu wake linaundwa na herufi nne za kaka na dada zake Rashid, Omar, Maimuna na Asha, ilimfanya arudi kwenye shule ya Sekondari ya Usagara aliyosoma miaka minne ya mwanzo ili kumalizia masomo yake ya kidato cha sita.


Roma anayejulikana kwa uvaaji wa rozali anasema mwaka 2007 ndipo aliamua kufanya muziki baada ya kuvutiwa na Profesa J.

Rhymes of Magic Attraction, kirefu kingine cha jina lake, kikathibitika kutokana na uandishi wake wenye meneno makali.

Anasema wimbo wake uitwao Pastor, ndio uliompa matatizo zaidi baada ya kuonekana umekaa kidini na kupendelea zaidi dhehebu la Roman Catholic kutokana na mstari unaosema, “Zitakuja dini zote lakini RC itabaki.” 

Radio nyingi ziligoma kuucheza wimbo huo na hivyo kudumu kwa miezi minne pekee.

Wimbo Mathematics ndio uliompa umaarufu maradufu baada ya kumpa tuzo mbili za Kili, mwanamuziki bora wa Hip hop wa mwaka 2011 na wimbo bora wa Hip Hop wa mwaka 2011.

Na sasa akiwa anajiandaa kuachia documentary yake, albam yake iliyoshirikisha wasanii kama Jos Mtambo, Izzo B, Mwana FA, Kala Jeremiah, JCB, Chiku Keto na wengine iko mbioni kutoka.