Jana mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba ya Tusker Project Fame msimu wa tano Linius ameyaaga mashindano hayo.
Akijaribu kuwashawishi majaji na walimu kwa mara nyingine baada kuwekwa kwenye probation, Linius aliimba wimbo wa Diamond ‘Mbagala’ ambao hata hivyo haukumwokoa.
Linius sio peke yake aliyeyaaga mashindano hayo kwani ameungana na wenzake wawili Brian Luzinda wa Uganda na Diana Teta wa Rwanda.
Washiriki walioponea chupuchupu usiku wa jana ni Doreen Muchiri wa Kenya, Nancy wa Sudan Kusini na Joe wa Burundi.