Rais Kikwete awaapisha mabalozi Kumi Ikulu jijini Dar es Salaam leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha mabalozi wapya kumi ambao wataongoza idara na kurugenzi mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Pichani Rais akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto walisimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha Semu Somi,Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana,Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz,Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari Msechu.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji,Balozi Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan Muombwa Haji(picha na Freddy Maro)