WANAFUNZI WA UDOM WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI LEO

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni  mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi na timu yake nzima wakati walikuja kufungua zoezi la kujitolea damu kwa hiari kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) zoezi lililoandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuoni Hapo
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
Baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao Pia Wamemaliza Muda wao rasmi leo Wakiwa katika zoezi la Uchangiaji Hiari wa Damu zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo ambalo liliandaliwa na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosoholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO). Kutoka Kushoto Ni Emmanuel Mwakibinga akifuatiwa na Stefano Saimon.
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo leo.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa http://josephatlukaza.blogspot.com
6/11/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0


Toa Maoni Yako Kwa Uhuru

Modified by MKCT

Idadi ya watu
Idadi ya watu