INIESTA MCHEZAJI BORA EURO 2012.
KIUNGO wa kimataifa wa
Hispania, Andres Iniesta ambaye ameisaidia timu yake hiyo kunyakuwa taji
la pili mfululizo la michuano ya Ulaya iliyofanyika nchini Poland na
Ukraine ametajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo. Iniesta ambaye
alitoa msaada mkubwa kwa timu yake ya Hispania katika nafasi ya katikati
na kupelekea kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 hivyo kuifanya nchi
hiyo kuwa ya kwanza kutetea taji lake kwenye michuano hiyo. Ofisa Mkuu
wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Andy Roxburgh
amesema kuwa kuna wachezaji wengi kama Andrea Pirlo wa Italia Xavi
ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita na Xabi Alonso walionyesha
viwango vizuri katika michuano hiyo. Lakini Iniesta alionyesha uwezo wa
hali ya juu zaidi ya wenzake hao kutokana na kuwa mbunifu, kasi na uwezo
binafsi pale timu yake inapokuwa katika wakati mgumu. UEFA pia iliteua
timu ya nyota wa Ulaya ambayo itaundwa na wachezaji kutoka nchi
mbalimbali zilizoshiriki michuano hiyo ambao ni makipa: Gianluigi
Buffon-Italia, Iker Casillas-Hispania, Manuel Neuer-Ujerumani, mabeki:
Gerard Pique-Spain, Fabio Coentrao-Ureno, Philipp Lahm-Germany,
Pepe-Ureno, Sergio Ramos-Hispania, Jordi Alba-Hispania. Wengine ni
viungo Daniele De Rossi-Italia, Steven Gerrard-Uingereza, Xavi-Hispania,
Andres Iniesta-Hispania, Sami Khedira-Ujerumani, Sergio
Busquets-Hispania, Mesut Ozil-Ujerumani, Andrea Pirlo-Italia, Xabi
Alonso-Hispania wakati washambuliaji ni Mario Balotelli-Italia, Cesc
Fabregas-Hispania, Cristiano Ronaldo-Ureno, Zlatan Ibrahimovoic-Sweden,
David Silva-Hispania.