Dk. Magreth Mtaki.
GUMZO
juu ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars kufanya
vitendo vya kustareheshana, limetetewa na baadhi ya wataalam kuwa ni
tendo linaloweza kufanyika kama lilivyo tendo lingine.
Mjadala
ulizuka wiki mbili zilizopita juu ya kufanya vibaya kwa Twiga Stars kwa
kufungwa jumla ya mabao 3-1 na Ethiopia katika mechi za kuwania kucheza
Fainali za Afrika zitakazofanyika Equatorial Guinea baadaye Novemba.
Mkwasa
alisema kuwa kufanya vibaya kwa timu hiyo kumechangiwa kwa kiasi
kikubwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kuendekeza vitendo vya
kusagana, lakini akasema kuwa waliokuwa wakifanya 'hayo mambo' (bila
kuwataja) walitimuliwa.
Lakini
vitendo hivyo vimetajwa kushamiri hasa katika timu zinazojumuisha
wanawake ama wasichana wengi kwani kila mmoja anakuwa na tabia na
mihemko yake kiasi cha kuwaathiri wengine.
Spoti
Mikiki ilifanya mahojiano na Dk. Magreth Mtaki, daktari wa michezo wa
siku nyingi kutoka Kurugenzi ya Michezo ambaye anasema kuwa kusagana
(lesbianism) ni kama starehe nyingine ambayo watu wa jinsi mbalimbali
wanafanya.
Anasema
kuwa tatizo linakuja kuwa ni suala linalohusisha wasichana ama kinamama
ndiyo maana linaleta mshangao, lakini hakuna tofauti na matendo mengine
ama kustareheshana kwa watu wawili.
Dk.
Mtaki ambaye pia ni Makamu wa Chama cha Soka ya wanawake Tanzania,
TWFA, anasema kuwa kitendo cha kusagana, kwa upande mwingine kina athari
kubwa kwenye timu kwani endapo kitafanywa kwa kuzidisha, inamaliza
nguvu mchezaji.
"Hata
ingekuwa wewe na mke wako, una mechi ya kimataifa ama ligi, halafu
ukafanya tendo la ndoa kupitiliza, ni wazi itapunguza uwezo wako
uwanjani, basi hata hawa wanaosagana, wakizidisha, lazima uwezo
utapungua.
"Kingine
ambacho naweza kusema, lakini sasa hii ni kwa mchezaji mwenyewe...hali
hii itamfanya hatokuwa na hamu ya mwanaume akiamini kuwa mwanamke
mwenzake anakata kiu.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz