Nyota
wanaofanya kweli kwenye gemu ya muziki wa kizazi kipya Bongo, Joseph
Rushahu’ Bwana Misosi’ Asleim Ngaiza ‘Soggy Doggy’ na D-nob wamenusurika
kifo na kulazimika kusitisha ziara yao ya kimuziki kwenye moja ya
visiwa ndani ya ziwa Victoria baada ya Boti waliyokuwa wakiitumia
kusafiria kupata hitilafu.
Akizungumza
na Teeentz.com via4n kutoka wilayani Kahama, Bwana Misosi amefunguka
kuwa wakiwa wilayani Muleba , walipanda boti maalumu kuelekea katika
moja ya visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria lakini muda mfupi baada
ya safari yao kuanza boti hiyo ilipata hitilafu.
soggy Dog kushoto
soggy Dog kushoto
“Ilikuwa ni wakati mgumu kwetu, boti ilipata hitilafu, tunashukuru Mungu jamaa wengine waliokuwa kwenye safari na boti zingine walifika na kutuokoa halafu ile tuliyokuwa tunatumia sisi ikavutwa na kurejeshwa mahali tulipoanzia safari” alisema Bwana Misosi.
Akiendelea zaidi Bwana Misosi aliarifu kuwa kutokana na ishu hiyo waliamua kusitisha ziara yao katika visiwa hivbyo na kurudi Muleba mjini kabala ya kukwea ndiga kuelekea wilayani Kahama kwa shoo nyingine.
STORI NA DISMAS TEN