olisi mkoani Mbeya inamshikilia Joseph Mtawa, kwa tuhuma za kumbaka binti yake anayemlea mwenye umri wa miaka saba.
Mtuhumiwa huyo mkazi wa kijiji cha
Shigamba Wilaya ya Mbeya Vijijini, alimbaka binti yake wa kambo baada ya
kumvizia mtoto huyo akiwa amelala sebuleni saa tano usiku .
Alidaiwa kuwa alimtoa binti yake sebuleni na kumpeleka kwenye pagare na kumfanyia kitendo hicho.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema mtuhumiwa huyo yupo rumande na
atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Ilielezwa kuwa tukio hilo liligunduliwa
na mama wa mtoto huyo mwenye miaka 27 (jina linahifadhiwa) ambaye
alipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani waliomkamata na kumfikisha
polisi.
Kamanda Athumani alitoa wito kwa wananchi
kuepuka vitendo vya udhalilishaji ambayo ni kinyume cha haki za
binadamu na ustawi wa watoto.
Mara nyingi matukio kama haya yamekuwa
yakitokea majumbani na yamefanywa na watu walio karibu na watoto ama
ndugu zao na yamekuwa yakihusishwa na ushirikina .