WAKATI
baadhi ya wabunge wakitaka kuwachukulia hatua Waziri wa Nishati na
Madini, Pofesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakimu Maswi kwa
madai ya kuiuka sheria ya Ununuzi wa Umma, mtendaji mkuu huyo wa wizara
ametupa kombora la ufisadi dhidi ya baadhi ya kampuni za mafuta
nchini.Wanaowatuhumu akina Muhongo na Maswi wanadai kuwa, walikiuka
sheria ya ununuzi wa umma kwa kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy ya
kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na
kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali
wa zabuni ya Tanesco.
Suala
hilo linahusishwa na kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,
William Mhando kwamba alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii
maelekezo ya Wizara.