MSANII Rehema Chalamila ‘Ray C’ au unaweza kumuita ‘kiuno bila mfupa’ utakuwa
haujakosea, amefunguka na kudai kuwa mikakati yake ya ndoa na bwana
ake wa Kenya bado inaendelea lakini wanaochelewesha ni wazazi wa
mwanaume ambao wanaonekana kuchukua muda katika kutoa maamuzi.Kufunguka kwa msanii huyo kumekuja siku chache baada ya kuzungumza na
mwandishi wetu, ambapo alidai kuwa hataki kufanya mambo haraka haraka
kwani muda bado upo wa kutosha.
Ray C stejini
Msanii huyo alipoulizwa kuwa tangu iliposikika anataka kuolewa huko nchini Kenya ni muda mrefu umepita ni kitu gani kinachokwamisha, alijibu kuwa kwa upande wake yupo tayari lakini upande wa mwanaume ndiyo wanaochukua muda kutoa maamuzi lakini anaamini kuwa kila kitu kitaenda kama walivyopanga.
“Kila kitu kinakuwa na mipango hivyo sitaki kufanya mambo haraka halafu mwisho wa siku watu waje kunicheka, eti ndoa yangu imevujika sitakimie,” aliongeza.