Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
MSANII wa filamu na muziki wa Pwani,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameponea chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani
maeneo ya Darajani mjini hapa baada ya kukatiza mitaa ya sokoni akiwa
katupia kigauni kifupi ajabu.
Bongowood ilimshuhudia Shilole akiwa na wanenguaji wake akipigiwa
kelele na wanaume waliotaka kumkamata wamvue kisha wamlambe viboko
hivyo akalazimika kukimbilia dukani akanunua dela na kulivaa juu ya
kigauni cha kihasara alichokuwa amekitinga.