Soka la Uingereza lahofiwa kugawanyika kutokana ubaguzi wa rangi

 

Kesi ya ubaguzi wa rangi iliyokuwa inamkabili nahodha wa zamani wa Uingereza John Terry, imesababisha mgawanyiko mkubwa kwa wachezaji wazungu na weusi nchini Uingereza.

John Terry alikuwa anakabiliwa na kesi ya kumtolea maneno ya kibaguzi mlinzi wa timu ya Queens Park Rangers Anton Ferdinand.
Kumekuwepo na makubalino miongoni mwa wachezaji wenye asili ya Africa kufanya mkutano wa kuanzisha shirikisho la kushughulikia ubaguzi wa rangi.
Kuna uwezakano mkubwa pia wachezaji wengi weusi wakakataa kushikana mikono na Terry kabla ya kuanza kwa mechi za ligi kuu.
Juzi kaka yake na Anton, Rio Ferdinand alijikuta lawamani pia baada ya kuchombeza ujumbe wa Twitter uliokuwa una lugha ya kibaguzi dhidi ya Ashley Cole wa Chelsea.
Ujumbe huo ulisema: “Looks like Ashley Cole’s going to be their choc ice. Then again he’s always been a sellout. Shame on him.”
Rio alijibu kwa kusema: ‘choc ice that’s a classic hahahaha.’
Mashabiki wa Chelsea wenye hasira na wadau wengine wa soka walimshambulia Ferdinand kwenye mtandao huo wa kijamii na kumshutumu kuwa na tabia za kibaguzi wa rangi.