BLATTER ASHANGAZWA NA UJERUMANI WALIVYOPEWA UENYEJI WA kOMBE LA DUNIA MWAKA 2006.


Sepp Blatter.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA amedokeza kuwa kuna uwezekano michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 nchi ya Ujerumani walipewa uenyeji kwasababu ya kutumia mlungula. Blatter mwenye umri wa miaka 76 alikumbushia kuwa mjumbe mmoja ambaye alikuwa na haki ya kupiga kura bila ya kutegemewa alijitoa katika chumba cha uchaguzi na anahisi kuwa hakuwa akijua kutofikiria lolote kwa wakati huo. Rais huyo wa shirikisho hilo amesema kuwa kama kuna nchi ilinunua kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia basi anafikiri itakuwa ni michuano ya mwaka 2006 wakati mjumbe mmoja alipoondoka ghafla katika chumba cha kupiga kura katika dakika za mwisho. Kwani alipoondoka mjumbe huyo ambaye alikuwa anafanya kura zilizopigwa zifungane na kuwa 10-10 kura zikabakia 10-9 na kuipa nafasi Ujerumani ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo. Kauli hiyo ya Blatter imeshutumiwa vikali na Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB ambacho kimedai kuwa rais huyo anataka kuzua jambo lingine ili kuzima kashfa ya rushwa ya sasa inayomhusisha rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange.