NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS
Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar
IKIWA
imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka
2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma
kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.
Kauli
za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea
huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo
kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.
Wakizungumza
katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma,
Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa
Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema
wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni
mzaliwa wa mkoa huo.
Katika
kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri
mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo
linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo
kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.
Akimzungumzia
kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana
lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi
yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo
kwa maslahi ya jamii.
"Lazima
mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote
bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba
tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi
yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:
"Vijana
wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka
michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."
Huku
akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa
Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na
wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe
alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".
Mbunge
huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika
mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais
kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao,
jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.
Chanzo