BAADA ya kusilimu na kupewa jina la Ilham Wolper Dallas, Jacqueline Masawe Wolper (pichani) amefunguka kuwa amejipanga vema na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaokuja.
Bongowood ilinasa sauti yake akihojiwa na Shadee wa Clouds FM ambapo staa huyo wa filamu alisema atahakikisha anafunga na kuvaa mavazi yanayostahili kwenye mfungo wa mwezi huo mtukufu.