Kwenye
U heard ya XXL Clouds Fm august 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown
ameripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa
saa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva
Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D amesema “kwa
nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli
sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi
sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo,
kwa sababu gani?
toka
nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe
kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha
mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna
taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari
sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”