FFU wakiwa wameuzuia msafara wa viongozi wa Chadema Taifa eneo la Miyomboni mjini Iringa jioni hii ,msafara huo ulikuwa ukitokea Morogoro kuja Iringa
Msafara wa Chadema ukiwa umepigwa Stop eneo la Miyomboni jioni hii
Jeshi la polisi mkoani Iringa limeuzuia kwa muda msafara wa viongozi wa kitaifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambao walikuwa wakiingia mjini Iringa wakitokea mkoani Morogoro.
Askari polisi hao wakiongozwa na askari wa FFU zaidi ya 100 waliuzuia msafara huo eneo la Zebra katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma baada ya jeshi hilo awali kuzuia maandamano ya Chadema na vyama vyote kwa maelekezo ya msajili wa vyama vya siasa.
Hata hivyo kutokana na umati mkubwa wa wananchi mkufika eneo hilo viongozi wa Chadema na polisi waliweza kukubaliana msafara huo kuendelea na safari yake kuelekea nyumbani kwa mbunge Msigwa eneo la Kihesa .
Katika tukio hilo jeshi la polisi halijaweza kutumia mabomu wala nguvu zaidi katika kuwatawanya wananchi kama ilivyo kuwa mkoani Morogoro jana.