Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’.
KATIKA
hali ya kushangaza, Mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Mathias Semagongo
‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa atatimka nchini kwenda kuishi
kusikojulikana.Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar, Aunt Lulu alifunguka kuwa
ameamua kukimbia mji kwani amechoshwa na manenomaneno ya walimwengu
jijini.“Nimechoshwa kwa kweli na kwa kuwa mipango yangu ya kuchomoka imetimia, acha nitimke Bango angalau nikapumzike kidogo nje ya hapa,” alisema Aunt Lulu pasipo kutaja anakotimkia.