ULE utata uliogubika kuhusu baba halisi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’, umetatuliwa na mama yake mzazi, Sanura Khassim ‘Sandra’ kwa kumtaja Nasibu Jumaa kuwa ndiye baba wa damu wa jamaa huyo anayekimbiza kwenye Bongo Fleva, Ijumaa Wikienda linashuka na stori kamili.
UTATA ULIPOANZA
Julai 16, mwaka huu, watu waliodai kuwa wao ni ndugu wa tumbo moja na Diamond waishio Kariakoo jijini Dar, waliibuka na kusema kuwa baba mzazi wa Diamond ni Salum Idd na alishafariki dunia tangu mwaka 2004 huku wakionesha vithibitisho vya picha.
CHANZO KIPYA CHAIBUKA
Agosti 9, mwaka huu, chanzo kipya kilicho karibu na mama Diamond kiliibuka na kudai kuwa mama Diamond alionesha kukasirishwa na habari ya utata wa baba Diamond iliyochapishwa gazetini na kudai ukweli halisi wa baba wa Diamond yeye ndiye anayeujua.
MAPAPARAZI MZIGONI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimsaka mama Diamond hadi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar ambapo bila hiyana Sandra alifunguka ya moyoni.
“Labda niwaambie tu kwa kifupi kama mama, baba halisi wa Diamond ni Abdul Jumaa kama ilivyokuwa inafahamika tangu awali,” alisema.
MAPENZI YAO
Mama Diamond alianika penzi lake na Abdul kwa kutiririka kuwa walikutana miaka kibao iliyopita wakapendana kupita maelezo ambapo mwaka 1989 walimzaa Diamond ingawa miaka michache baadaye, walimwagana huku chanzo kikielezwa kuwa ni mama mkwe kumkataa mama Diamond lakini bado wanapendana.