Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo jana kiliendelea kulalamikiwa na
Watanzania kwa kukosa DIRA ya uongozi hasa baada ya
kujichanganya,kubishana wenyewe kuhusu msimamo wa SERA yao hapa UK.
Haya yaliwakuta katika kikao cha kutafuta wanachama kilichofanyika jana
tarehe 27/08/2012 katika Mji wa Reading, UK.
Watanzania
wachache waliohudhuria mkutano huo walinung'unika kuwa kikao hakikuwa
na utaratibu na mtirirko wowote wa uendeshaji wa vikao na ulibagua
uchangiaji wa kijinsia na ulijali zaidi ukabila.
Akilalamika
huku akitoka nje ya ukumbi ndugu aliyejitambulisha kuitwa Said alisema
kuwa Kikao hiki kiliandaliwa kwanza na Wachaga tu waliochangishana
fedha na hivyo wakati wa kikao hawakutoa nafasi huru kwa watanzania
wengi kushiriki kikamilifu zaidi ya kuambiwa watoe fedha kuchangia
Chama na mfuko wa kuzikana.
Mwingine
ni Bi Rehema aliyesema kuwa ameshangazwa na kauli ya Bw. Prudence
aliyesema kuwa yeye ndiye ameachiwa jukumu la kueneza Sera na Siasa za
CHADEMA na hivyo ni lazima achangishiwe fedha za kuzunguka UK ili aandae
akina mama wasomi wajiunge Chadema ili wapewe nafasi za Ubunge wa Viti
Maalum katika uchaguzi mpya 2015 maana wengi wa waliopo muda wao
umekwisha na kuwa Viongozi wa Chadema wanajali kundi la akina mama.
Nanukuu..''eti
anatuambia mambo ya viongozi kujali wanawake na siyo Sera ya Chadema
juu ya wanawake...yeye mwenyewe ametelekeza mke na watoto wake
bongo..wanaomba omba tu huko yeye anakula raha na bado anataka michango
yetu zaidi....jana tu alikuwa ndiyo kada mwandamizi wa CCM hapa UK
akatengwa kwa sababu ya tabia zake...sisi siyo wajinga bwana..''
Ramadhani
aliongea kwa mfadhaiko akishangaa kuwa Dkta Jona LUSINGU ni Wakala wa
Chadema huku alikuwa ni Kiongozi wa Jumuiya ya Tanzania UK aliyeshindwa
kazi na kukimbia uongozi mwenyewe bila kukabidhi ofisi na sasa
atawezaje kusimamia siasa za Chadema ..''au ndiyo kuyeyushana tu..''.
Alihamaki akiwa anatoka mlangoni na kuunyosha mkono kuelekea kwa Dk
Lusingu aliyekuwa amekataliwa nafasi ya kukaa meza ya viongozi na hivyo
kukaa na washabaki wachache waliokuwepo.
Alipopewa nafasi ya kuongea Dkt Lusingu alizidi kuwachanganya viongozi na mashabiki wachache waliohudhuria pale aliposema ''Chadema
imekuwa haina sera ya Diaspora na Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa
na Chadema kuingia madarakani Tanzania na hasa uongozi wao wa kitaifa
uliopo sasa isipokuwa pale ambapo mfumo mzima wa utawala
utakapobadilika na chadema kuwa chama cha kitaifa kuliko hivi sasa''.
Aliongeza
kwamba matawi ya nje ya Chadema yanaweza yasiwe na manufaa iwapo kama
yatatelekezwa kama walivyofanya CCM.Aliongeza kuwa ni kweli toka
Chadema imekuja hapa UK kumekuwepo na manung'uniko miongoni mwa
Watanzania na ni vema kujipanga upya na uongozi msafi. Dkta Lusingu
aliyekatishwa kuongea alikuwa ni mmoja wa viongozi wa awali wa shina la
CCM Reading
MwanaCCM
mmoja anayeitwa Chris alidokeza kuwa waliohudhuria mkutano huu sehemu
kubwa ni wanaCCM walioingia kusikiliza kipya gani watani wamefuatia
nazo nyayo lakini wameona hakuna jipya bali maumivu ya kukosa SERA.
Alisema
kuwa CCM UK imekuwa na mapendekezo mengi katika vikao vya Taifa na
serikali imeanza kushughuliia kero nyingi za wanaDiaspora ikijumuisha
kumalizia mpango mahsusi wa kueneza na kuleta UK huduma za kifedha na
hifadhi za jamii kuliko danganya toto ya Chadema ya kuchangia mfuko wa
mazishi..
''yaani chadema wanaona umuhimu wa Mtanzania pale anapokufa tu na wao kumzika..'' Alidokeza kuwa ni uonevu kumtwisha mdogo wake Dkta Lusingu mzigo wa Chadema wa kuchangia vifo.. ''Wakati
Jeladi Lusingu alipofiwa na mkewe ni wanaCCM waliongoza kuhimiza kufa
na kupona miji yote ya UK ili kusaidia safari na hifadhi ya mwisho ya
mama huyo. Leo sera za umoja zilizomsaidia anazipinga au amelazimishwa
tu?''
Baada
ya kikao kuisha Bw. Prudence alitamba kwa wenzake kuwa alipokuwa CCM
UK kila mkutano walikuwa wakichangishana ili kuhudumia kikao na usafiri
na sasa wanachama wamechoka kifedha na hivyo sasa Chadema imeanza
kumwaga pesa kuwamaliza CCM kabisa hapa UK. Prudence alipoombwa
mahojiano ya ana kwa ana alisema hana muda.
Mwandishi
alitafuta na kupatiwa namba ya simu ya Mwenyekiti wa CCM UK ili kupata
mawazo yake juu ya mkutano huu wa Chadema hapa Reading lakini alisema
yupo Edmonton, London kuhudhuria CCM UK
BBQ-Outreach
Party iliyoandaliwa na wanaCCM North London tangu miezi miwili
iliyopita hivyo asingeweza kuahirisha lakini anayo nafasi ya mahojiano
baada ya siku hiyo. Pia alisema CCM ilikaribisha upinzani Tanzania na
inaendelea kuikaribisha Chadema hapa UK.
Na Mwandishi wa kujitegemea,
Clement Mbawala.
Tanzania Now.
Slough.Berkshire.