Diamond ameamua kutanua mabawa yake zaidi mwaka huu kwa kumshirikisha msanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria, J.Martins. Tayari amesharekodi sehemu zake kwenye wimbo huo kwenye studio za MJ Records chini ya producer Marco Chali.Habari zinadai kuwa kwa sasa wimbo huo
upo kwenye hatua ya final mixing ambapo chorus ya wimbo huo imeimbwa na
Diamond na dancer wake Mose Iyobo. Katika kuonesha kuwa bega kwa bega
na madancer wake, Diamond ameamua kumpa shavu Mose ambaye ameonesha
uwezo mzuri wa kuimba.
J.Martins ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akichukua kozi maalum ya miezi mitatu ya masuala ya utayarishaji, tayari anausubiri wimbo huo ili aingize sauti yake.
Katika hatua nyingine Diamond anaelekea mjini Washngton DC nchini Marekani kwaajili ya show. Kwenye safari hiyo Diamond anaenda na madansa wake wote wanne na msemaji wake.
Kwa mujibu wa Power Jams ya East Africa Radio, Diamond atafanya show kwenye mkutano mkubwa unaofanyika Marekani ambao wahudhuriaji wamemtaka akawape burudani.