Wiki hii kwenye kipindi kipya cha radio cha Makutano Show kinachorushwa kila siku za Jumamosi kupitia Magic FM, mmoja wa mabosi wa Clouds FM Ruge Mutahaba atahojiwa na mtangazaji wa show hiyo Fina Mango.
Kwa
namna yoyote interview hiyo itavuta wasikilizaji wengi hasa kwakuwa
Fina atakuwa akimhoji bosi wake wa zamani kipindi anafanya kazi Clouds
FM.
Licha
ya Fina Mango kuachishwa kazi pamoja na Masoud Kipanya, bado ameendelea
kuwa karibu na Ruge ambao wanamiliki pamoja kampuni ya One Plus
Communication.