Aliyekuwa
mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Garder G Habash aka
Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu ijayo kupitia kituo
cha radio cha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam.
Kipindi chake kiitwacho Maskani kitakuwa kikiruka kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.
Kuna
tetesi za mtaani ambazo hazijathibitishwa rasmi zinazosema kuwa
mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi.
Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM |
Kama tetesi hizo zitakuwa na ukweli, Gadner atakuwa mtangazaji wa radio anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini.
Kipindi
chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kipindi chake cha
zamani, Jahazi cha Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord
Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na Ephraim Kibonde.
Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa mingine ambayo Times FM haisikiki.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM. Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.
|