MADAMU RITA AOMBWA UCHUMBA NA ‘SERENGETI BOY’

Rita Paulsen ‘Madam Rita’.
CHIEF Judge wa Shindano la Epiq Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ hivi karibuni amejikuta akiombwa uchumba na vivulana nyenye umri mdogo ‘serengeti boys’ kupitia ukurasa wake wa Facebook.Akipiga stori na Mwandishi wetu , Madam Rita alisema kuwa, alianzisha ukurasa huo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na watu mbalimbali lakini akashangazwa na baadhi ya wavulana ambao wamempenda kiasi cha kufikia hatua ya kumuomba uchumba.

“Huwezi amini sina siku nyingi sana tangu nimeanzisha ukurasa huu lakini nina marafiki wengi na wapo ambao wanaomba kuwa marafiki wangu, huko nimeshapata wachumba sita tena wengine wakiwa na umri mdogo sana,” alisema Madam Rita na kuongeza:


“Kimsingi nawaheshimu watu wa rika zote kutoka mikoa yote kwani wao ndiyo wadau wakubwa wa EBSS na wameifanya program hii kujipatia umaarufu mkubwa na kufika hapa ilipo sasa.”