Jennifer
Kyaka ‘Odama’ amefunguka na kuweka wazi kuwa katika mafanikio
aliyoyapata hakuna mkono wa mwanaume kama ilivyo kwa wasichana wengine
mastaa wa mjini.Odama ameeleza kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii na kile
anachokipata ndicho anachofanyia mambo yote ya maendeleo ambapo hadi
unaposoma hapa, anamiliki kampuni yake ya filamu ya J-Film For Life,
magari mawili na mjengo.
“Mafanikio yangu yametokana na kazi zangu mwenyewe na hakuna mkono wa mwanaume, sitaki iwe hivyo ‘coz’ ndiyo maisha niliyoyachagua ya kutomtegemea mtu kwani kile ninachokipata kwenye filamu zangu ndicho kinachonipa maendeleo haya,” alisema Odama.
Hata hivyo, mwanadashosti huyo alisema kwa sasa ana mchumba na anatarajia kufunga ndoa mwakani.