SIKU
chache baada kukanyaga ardhi ya Bongo kutoka uhamishoni nchini Kenya,
nyota wa muziki wa kizazi kipya Afrika mashariki Rehema Charamila
amesema kuwa hajarejea nchini kusaka wanaume.
Akizungumza
juzikati jijini Dar Ray C amefunguka kuwa hakuja Tanzania kutafuta
Bwana wa Kuolewa nae kama watu wanavyovumisha mitaani isipokuwa
amefanya hivyo kwa ajiri ya mapumziko na kazi pia.
"Unajua
mimi niliamua kuhamia Kenya baada ya kuona kuwa ninsupport kubwa kwa
Mashabiki wa huko kuliko hapa Tanzania hivyo nikaamua kwenda kuwapa
kile wanachokipenda na pia kujaribu kukuza muziki wangu.
Katika kusibitisha hilo hivi karibuni natarajia kuachia ngoma yangu mpya amabayo nimeipa jina 'Moyo Waniuma' alisema Ray C.
MPAKA SASA RAY C HAJAZUNGUMZA LOLOTE JUU YA MADAI YA KUTOA MKANDA WA X AKIWA HUKO KENYA