Dully Sykes hajaacha tabia yake ya kujisifia ndo maana mama yake alimpa jina la Mr. Misifa.
Akiongea na Clouds FM msanii huyo mkongwe amesema yeye ni msanii wa kwanza nchini kupanda ndege.
Anasema
anakumbuka ilikuwa mwaka 2000 alipanda ndege kuelekea Mwanza ambapo
alikaa jirani na Joseph Kusaga ambaye alimwambia Dully asiogope ndege
kutokana na kuwa mgeni kwenye chombo hicho.
Dully pia ambaye kwasasa ameongeza aka mbili ‘Superstar na Hunter’ amesema yeye ni superstar wa kwanza Tanzania baada ya Profesa Jay.
Amesema
mwaka ambao Profesa aliachia wimbo wa Chemsha Bongo ndio mwaka aliotoa
wimbo wake Julietha na kusema yeye ndiye aliyeitambulisha Bongo Flava
nchini.