Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, akizungumza na mtandao wa Thehabari.hivi karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitopeni kutoka Wilaya ya Korogwe.
“Mabadiliko
ya mitaala na mchanganyiko wa vitabu bila utaratibu mahususi ni tatizo,
kwa sasa hivi kila shule ina kitabu chake katika somo fulani…hata hivyo
licha ya mabadiliko ya mara kwa mara hakuna maandalizi, mimi tangu
nimalize chuo 1979 sijaenda semina yoyote wala mafunzo kujiandaa na
mabadiliko ya mitaala hii. Hili linachangia pia,” alisema mwalimu Mtui.
Akifafanua
zaidi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Muungano, ya wilayani
Moshi, Ashati Elihaki alisema mbali na mchanganyiko juu ya suala la
vitabu vya masomo mabadiliko ya mitaala yamegeuza baadhi ya masomo
kubaki kama ‘kiini macho’ jambo ambalo ni tatizo kwa walimu.
“…angalia
kwa mfano somo kama la Tehama linaloanza kufundishwa darasa la tatu
hadi la saba somo hili lipo kinadharia zaidi, hakuna walimu ambao
wameandaliwa kufundisha somo hili lakini linatakiwa kufundishwa eti kwa
kutumia mwongozo wa mwalimu kimsingi hii si sawa,” alisema Elihaki.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, Theodolph
Karigita alisema tofauti na ilivyokuwa hapo awali mitaala ya sasa
imevurugwa kiasi kikubwa jambo ambalo linawachanganya walimu na hata
wanafunzi hivyo kushindwa kufanya vizuri.
“…Mitaala
imevurugwa sana, kunamchanganyiko wa masomo nadhani unakumbuka kuna
kipindi baadhi ya masomo yaliunganishwa kama Jiografia, Historia na
Uraia wakaita maarifa ya jamii…kipindi hiki wanafunzi walifanya vibaya
sana hivyo ikabadilishwa sasa watoto wanafanya vizuri tofauti na awali,”
alisema Karigita.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, Youze
Mbwambo alisema idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza
hadi la tatu ni chanzo kingine cha wanafunzi hao kufanya vibaya kwani
wamekuwa wakibebeshwa mzigo pasipo sababu za msingi.
Akizungumzia
hoja hizo zilizotolewa na baadhi ya walimu, Ofisa Elimu Taaluma,
Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Elius Mkwizu alisema mabadiliko
yanayofanywa na wataalamu hufanywa kwa malengo mazuri licha ya kuwepo na
changamoto kadhaa maeneo tofauti.
Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Taasisi ya HakiElimu.