Maisha
Plus is back na shughuli ya kusaka washiriki wa kuingia kijijini
mwezi October utaanza rasmi siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya usaili.Tofauti
na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika
vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula wapatao 15 walipatikana kutokana
na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza la
Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.
“Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26", Masoud Kipanya ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo.
Mshindi wa mwaka huu atakamata kitika cha shilingi milioni 20.