NILIKUWA NIMESHAZIBA PENGO LA VAN PERSIE - WENGER.
KOCHA wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa hatanunua mshambuliaji mwingine
ili kuziba pengo la nahodha wake aliyeoondoka Robin van Persie. Klabu
hiyo ilifikia makubaliano na klabu ya Manchester United juu ya uhamisho
wa mchezo wa mchezaji kwa ada ya paundi milioni 24 lakini Wenger amesema
kuwa tayari alishapata mbadala wa Van Persie wakati alipowasajili
Oliver Giroud na Lukas Podolski. Wenger ambaye ni raia wa Ufaransa
amekiri kuwa klabu hiyo ilikuwa haina jinsi zaidi ya kumuuza
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ambaye alikuwa amebakisha
mwaka mmoja. Kocha huyo amesema kuwa huwa inaumiza kumkosa mshambuliaji
mwenye kiwango kama cha Van Persie lakini walikuwa hawana jinsi kwakuwa
mshambuliajihuyo alikuwa amebakiza mwaka mmoja na hakutaka kusaini
mkataba mwingine.