Operesheni Sangara-Kijiji Cha Singisa, Jimbo La Morogoro Kusini



Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akionyeshwa madarasa ya Shule ya Msingi Singisa. Hii ni shule pekee ya katika kijiji hiki ambacho ni makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa
Ofisi ya Kijiji na Kata ya SINGISA Jimbo la Morogoro Kusini Katika Taswira. Katibu.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akionyeshwa sehemu ya vyoo vya wanafunzi wa shule ya SINGISA

Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi akiwa na wanakijiji wa SINGISA jimbo la Morogoro Kusini katika ofisi ya mwalimu wa shule hiyo

Na: Mdau Hellen Dalali

Operesheni Sangara zinazoendelea Morogoro bado zimeendelea kuwa chachu ya kuimarisha CHADEMA katika kila vijiji wanavyofikia. Picha hizi ni katika kijiji ambacho hakuna zahanati na kina shule moja tu ya Msingi yenye wanafunzi 398 na Mwalimu mmoja tu!!Wanafunzi wote wanakaa chini.

Kijiji hiki ifahamike ndicho pia makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa.(Kata ya Singisa ina vijiji 7). Makao Makuu ya Kata ndipo pia mwisho wa barabara, hivyo vijiji vingine sita havifikiki na vimetengwa kabisa kimawasiliano.

Moja ya lalamiko kubwa la wananchi, wamekuwa wakichangishwa michango isiyo na idadi na serikali ya kijii huku wakiwa hawasomewi mapato na matumizi. Baada ya elimu hasa ya uraia na umuhimu wa haki yao hiyo iliyotolewa na CHADEMA, wanakijiji wameapa ndani ya wiki mbili wataitisha mkutano wa kijiji na kuwatimua madarakani viongozi wa kijiji baada ya kuenda kinyume na taratibu za kuendesha serikali ya kijiji.