"SIKUMBUKI IDADI YA WANAUME NILIOFANYA NAO."......AUNT LULU

MWANADADA asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ ametoa kali ya mwaka na kusema kuwa hajui idadi ya wanaume alioshiriki nao kimapenzi kwa kuwa ni wengi.Anti Lulu amesema amefanya hivyo kwa kushirikiana na wanaume mastaa na wasio mastaa hali ambayo huwa inasababisha asikumbuke idadi yao.

“Kwa kweli sikumbuki, ila ambaye nilidumu naye muda mrefu kiasi ni Bondi ambaye ndiye alinivalisha pete, lakini niliivua baada ya kunipiga na kunipasua usoni,” alisema Lulu ambaye alipata umaarufu kupitia shindano la kucheza la Kimwana Manywele 2006 kabla ya kuhamia kwenye uigizaji filamu.