Rose Muhando
Malkia
wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando hatimaye amemaliza
kurekodi album yake mpya ya sauti pamoja na kurekodi nyimbo mbili kwenye
video huko nchini Afrika ya kusini chini ya kampuni ya Sony Music
Entertainment ya Afrika ya kusini.Kwa mujibu wa taarifa alizotoa mwimbaji huyo hivi karibuni amesema
amekamilisha nyimbo tatu zilizokuwa zimebakia katika kukamilisha album
hiyo ya sauti ambayo hata hivyo hajaitaja jina.Mwimbaji huyo ambaye aliingia mkataba na kampuni hiyo ya kimataifa mapema mwaka jana, tayari amepata mafanikio makubwa kwenye medani ya muziki wa injili nchini tokea atoe album yake ya kwanza ya ''Mteule uwe Macho'' hadi yasasa ya ''Utamu wa Yesu''.
Hapana shaka kwamba album mpya itakuwa na kiwango kikubwa zaidi cha usikivu si kwenye sauti tu pia muziki wake utakuwa umerekodiwa kwenye viwango vikubwa kitu ambacho kitalifanya jina la Kristo lizidi kutangazwa si Tanzania tu bali maeneo mbalimbali duniani. Kila la kheri Rose Muhando.