DOGO JANJA NA MADEE WASAMEHEANA.....

RAPA katika medani ya Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amesema hana bifu na mkongwe katika tasnia hiyo, Hamad Ally ‘Madee’ na kudai kuwa yupo tayari kufanya naye kazi.
Wawili hao walikuwa na tofauti siku za hivi karibuni kutokana na Dogo Janja kujitoa kwenye familia ya Tip Top Connection na kukwaruzana na Madee, ambaye ndiye aliyemkaribisha kwenye familia hiyo awali.

Namuheshimu sana, Madee ni kaka yangu na sina bifu naye licha ya matatizo yaliyotokea hivi karibuni, nipo tayari kuimba nyimbo moja ya kushirikiana pamoja na kupanda jukwaa moja,” alisema Dogo Janja.