‘Sintah’ na mwanadada Agnes Gerald sasa wamekubaliana na kusamehana ishu picha za utupu


BAADA ya mvutano juu ya ishu yao ya kuweka picha za utupu kwenye mitandao msanii Christine John  ingawa wamewekeana mipaka ya kupigiana simu nyakati za usiku kwani kila mtu huwa anafanya mambo yake.
Mtandao wa DarTalk, ulizungumza na wasanii hao ili kujua kipi kinachoendelea baada ya kutofautiana kutokana na ishu iliyokua inachukua sura mpya kila siku bongo baada ya watanzania wengi kuziona picha za utupu za mwanadada Anges zilizodaiwa kuwekwa na Sintah kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo kwa upande wake Sintah, alidai sasa hawana tena bifu na walikutana ili kujandili ishu hiyo ambapo sasa wote wamekuwa kitu kimoja, na hawakumbuki kama walikuwa na utofauti.


“Sisi ni wanadamu hivyo tunamezungumza na sasa hatuna tena bifu, ingawa ni kweli mambo yalikuwa mabaya ila kwa sasa hakuna kitu kinachoendelea zaidi ya kujenga urafiki, pengine nachoweza kuongeza ni kwamba nampenda sana Anges ingawa kuna muda tabia zake zinakera,” alidai.


Hata hivyo aliongeza kuwa baada makubaliano yao wamepanga kucheza filamu moja.


Naye Agnes alidai kuwa baada ya kuona hawawezi kupata muafaka waliamua kukutana na kuzungumza kwani sasa wamekuwa kama ndugu na kuondoa ubishi wao wote uliokuwepo, ingawa alijisikia vibaya baada ya picha zake kuonekana kwenye mitandao bila ruhusa yake.


Hata mwandishi alipomuuliza kuwa ule mpango wake wa kutaka kuzianika picha za utupu za Sintah kwenye mitando umefikia wapi, au urafiki alioanzisha ni njia moja wapo ya kutafuta picha za Sintah akiwa mtupu, alijibu kuwa hayo ameshasahau na anachofikiria sasa ni kujenga urafiki na kufanya vitu vya kimaendeleo