JINI KABULA: Sikumpenda Mr Nice Kabisa
STAA wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa
hakuwahi kumpenda Mbongo Fleva, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ndiyo maana
hakumzalia mtoto kama ilivyokuwa kwa wanaume aliowapenda.Akizungumza na Mbovumbovu za Mastaa, jijini Dar hivi karibuni, Jini
Kabula aliweka ‘plain’ kuwa akiwa katika uhusiano na mwanaume
anayempenda lazima amzawadie mtoto hivyo kipindi ‘anatoka’ na Mr Nice,
(miaka kadhaa iliyopita) hakuwa amempenda ndiyo maana hakuzaa naye.
“Nilizaa na Chuzi kwa sababu nilimpenda, sasa nina ujauzito wa Bushoke nitazaa naye kwa sababu nampenda,” alisema Jini Kabula.