WAKATI wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi mwaka huu wakiwa wamepata watoto, naye Wema Sepetu ameweka
wazi kuwa anahitaji mtoto na anafikiria kuzaa na kijana mdogo wa umbo
anayetesa kwenye game la muziki wa kizazi kipya bongo, Nasseb Abdul ‘Diamond’.Wema, alifafanua kuwa anatamani kuitwa mama kwani mbali na hilo pia umri
wake unazidi kusogea. Alidai kuwa ndani ya mwaka 2013 anatarajia
akamilishe ishu hiyo kwani wapo baadhi ya rafiki zake ambao wana watoto
na anajisikia aibu pale anapokutana nao wakiwa na watoto wao.
“Sina tatizo juu ya hilo, sasa ninaweka wazi kuwa nahitaji kuwa na mtoto lakini na katika kukamilisha malengo nataka kumpatia mtoto Diamond ingawa tulishawahi kuwa matatizo ya siku za nyuma baadhi ya watu wakadai kuwa nimetoa mimba,”. alisema Wema
Mwandishi wetu alipomuliza Wema kuwa endapo akiwa na mtoto vipi suala zima la kula bata na kujiachia, alijibu kwa mkato kuwa hilo litaendelea lakini mwanaye atamlea kama alivyolelewa yeye na mama yake.