NISHA NA NAY WA MITEGO SASA NDANI YA PENZI ZITO


STAA wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’ na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elbariki ‘Nay wa Mitego’ sasa wapo ndani ya penzi zito.Chanzo chetu cha kuaminika kimetutonya kuwa, wawili hao wameingia kwenye uhusiano wa kimapenzi miezi kadhaa iliyopita na sasa wameamua kuliweka penzi lao hadharani.

“Zamani Nisha alikuwa anafichaficha lakini sasa kila kitu kipo hadharani na hakuna kificho, wanaishi kama mke na mume kwa jinsi wanavyopeana kampani,” kilisema chanzo hicho.

Kwa nyakati tofauti wawili hao walipotafutwa na Mwandishi   wetu, kwa pamoja walikiri kuwepo kwa uhusiano ‘hot hot’ wa kimapenzi na kudai kuwa dhamira ni kuoana.

“Ni kweli mimi na Nay ni wapenzi na naamini uhusiano wetu hautaishia njiani kama inavyokuwa kwa wengine,”
alisema Nisha huku akionekana ni mwenye imani kubwa kwa Nay.