AIBU: KUMBE ALIYEPIGA PICHA ZA NUSU UCHI NA CHAMELEONE NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA NKUMBA

Hivi karibuni tuliweka picha ya aibu inayomwonesha mrembo mmoja akiwa na Jose Chameleone wa Uganda kwenye pozi la zero distance.

Picha hiyo inamwonesha msichana huyo akiwa hajavaa nguo ya ndani huku nguo ya juu aliyokuwa amevaa kuishia chini ya kiuno na hivyo makalio yake kuonekana nje.

Picha hiyo imezua mjadala mkubwa nchini humo kwa jinsi dada huyo alivyotia aibu.

Well, msichana huyo ni supastaa nchini Uganda. Ni model mwenye miaka 22 aitwaye Doreen Kabareebe.



Aliwahi kushiriki shindano la Miss Uganda 2010, Miss Inter-Universities na Miss Central University ambako alishinda taji kutoka Nkumba University.



Ni mwanafunzi wa Public Administration katika chuo kikuu cha Nkumba mjini Entebbe.

Ni msichana ambaye haipiti siku bila kuandikwa kwenye magazeti ya udaku ya nchini humo kwa tabia yake.