WILSHERE KUPEWA JEZI NAMBA 10.
KIUNGO wa kimataifa wa
Uingereza na klabu ya Arsenal Jack Wilshere anatarajiwa kupewa jezi
namba 10 ambayo alikuwa akivaa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo
aliyehamia Manchester United, Robin van Persie. Wilshere
amekuwa nje uwanja kwa kipindi cha miezi zaidi ya 12 kutokana na
majeraha yanayomsumbua atapewa jezi hiyo ambayo mbali na kuvaliwa na Van
Persie lakini pia imewahi kuvaliwa na nyota wa kimataifa wa Uholanzi
Dennis Bergkamp. Kiungo
huyo anaelekea kupona kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu ambayo
yamemsumbua kwa kipindi kirefu sasa na anatarajiwa kurejea dimbani
Octoba mwaka huu. Kwa
upande mwingine meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesikitishwa na
kitendo cha kumuuza mchezaji huyo ambaye pia alikuwa nahodha wake kwa
mahasimu wao United na kukiri kuwa afadhali angemuuza sehemu nyingine
lakini sio Uingereza.