Aunt Ezekiel.
MSANII wa picha
za Kibongo, Aunt Ezekiel anadaiawa kutiwa mbaroni kwa utapeli wa Sh.
miloni moja alizopewa kwa ajili ya kucheza filamu.Kwa mujibu wa
mlalamikaji, Mwajuma Said ambaye alimsainisha Aunt mkataba wa kucheza
filamu yake ya That’s the Long Story, walikubaliana kuanza kucheza
filamu hiyo Juni 2, mwaka huu lakini Aunt hakutokea na baada ya
kuwasiliana naye ndipo akadai ana dharura ya safari ya kwenda Dubai.Baada ya mwigizaji huyo kuzingua, Mwajuma alikwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni, Dar ambapo Aunt alisakwa na kufikishwa kituoni hapo.
Alisema kuwa baada ya bidada kukiri ‘kuchikichia’ mshiko huo, alikubali kutoa Sh. laki sita na kubaki na deni la Sh. laki nne ambazo aliomba kuzilipa akirejea kutoka Dubai.
“Alipotua kutoka Dubai nilimtafuta nikamuuliza akawa ananijibu majibu yasiyoeleweka, ikabidi nirudi polisi ambapo walifika nyumbani wakamkosa lakini wakamtafuta hadi wakamfikisha kwenye Kituo cha Magomeni, Dar na akatoa Sh. laki mbili,” alisema Mwajuma.
Ilisemekana kuwa baada ya Aunt kutoa laki mbili na kubaki na deni la laki mbili aliahidi kumalizia deni kesho (Jumanne) na nakala za makubaliano tunazo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walimtafuta Aunt ambaye alidaiwa kuishiwa na utoto wa mjini na kuwa mdogo kama kidonge cha piritoni ambapo hakupatikana kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa meseji hakujibu.