Good Girl Gone Bad, Rihanna hivi karibuni kidogo atupwe nje ya klabu ya jijini London baada ya kupanda kwenye meza.
Muimbaji huyo mwenye miaka 24 alikuwa akijirusha kwenye klabu ya The Rose iliyopo kwenye mji huo mkuu wa Uingereza, baada ya kupanda juu ya meza na mabaunsa waliokuwa na hasira kutaka kumbeba mzobe mzobe hadi nje.
Bahati ni kuwa marafiki zake waliingilia kati na Rihanna kujifagilia kwa sauti “Don’t you know who I am?”.
Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun: “They were trying to eject her when her girlfriends starting screaming, ‘That’s Rihanna, you idiots!’
Mabaunsa hao ambao bahati mbaya hawakuwa wakifahamu kuwa huyo ni Rihanna walimshika kumtoa nje lakini kabla hawajafikia kwenye mlango wa kutoka waligundua kuwa wamefanya kosa na meneja wa klabu huyo alitembeza vinywaji vya bure kwenye meza ya muimbaji huyo.