IRINGA KIMENUKA: MWANDISHI WA HABARI AUAWA NA POLISI MMOJA YUKO MAHUTUTI.. CHANZO NI VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI

Habari zilizotufikia hivi  zinasema kuwa, Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi (pichani) wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten amefariki dunia katika ghasia zilizozuka kati ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na polisi katika mkutano wa chama hicho mkoani Iringa .

Pia askari polisi mmoja wa Wilaya ya Igowole anasemekana yuko mahututi kutokana na kipigo. Taarifa kamili kuhusiana na tukio hili zitawajia baadaye.