Prezzo na waziri mkuu Raila Odinga walipokutana hivi karibuni |
Mwamko
wa wanamuziki vijana kujiingiza kwenye siasa haupo Tanzania pekee.
Kenya mambo ni yale yale pia. Miongini mwa wasanii walioonesha dalili za
kupanda kwenye majukwa ya kisiasa nchini humo ni Prezzo na Jaguar.
Siku
chache baada ya kuwasili nchini Kenya, Prezzo alipata fursa ya
kukutana na waziri mkuu Raila Odinga kwa mazungumzo ya siri.
Hakuna
anayejua walizungumza nini lakini wengi wanaamini Raila aliutumia
mkutano huo kumpongeza kwa kuiwakilisha nchi yake kwenye BBA na kumpa
dondoo kadhaa za namna ya kuwa mwanasiasa aliyefanikiwa.Mazungumzo hayo
yalimalizika kwa wote kupiga picha ya pamoja
Jaguar na Raila Odinga hivi karibuni |
Haujapita
muda mrefu, Jaguar naye akamzukia Raila ofisini kwake. Huenda ikawa ni
tukio la siku moja kwakuwa Raila anaonekana kuwa na suti na tai ile
ile. Jaguar na Prezzo wanaweza wasigombee uongozi wowote kwenye
uchaguzi ujao, lakini wameanza kujiweka karibu na manguli wa siasa ya
Kenya ili kujisafishia njia mapema.
Kwa
haraka haraka, kinachokuja akilini mwetu hapa ni kuwa labda Raila
Odinga anataka kuwatumia wasanii hawa wote kwaajili ya kumpigia kampeni
kwenye uchaguzi ujao wa urais nchini humo.
Wote
wakiwa kwenye kambi moja, kuna mvuto mkubwa utakaoonekana kwenye
kampeni ya Raila hasa ukizingatia kuwa wasanii hawa walikuwa maadui
wakubwa.
You
never know, pengine kuna mpango wa kufanyika ngoma ya pamoja ya wakali
hawa itakayompigia debe mgombea huyo wa urais. Muda utaongea.